Askari Polisi afia Bar akiwa tungi kichwani, wahudumu waeleza kilichomsibu dakika za mwisho - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Askari Polisi afia Bar akiwa tungi kichwani, wahudumu waeleza kilichomsibu dakika za mwisho

Askari Polisi mmoja mkoani Ruvuma, amekutwa amekufa kwenye Bar ya Friend’s Pub  iliyoko katikati ya mji wa Songea huku ikielezwa kuwa alikuwa amekunywa pombe kupita kiasi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Machi 15, 2019 ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma,  Simon Marwa, alimtaja askari polisi aliyekutwa amekufa kuwa ni Konstebo Donald Motoulaya (29), ambaye ni askari katika ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa.

Kamanda Marwa amesema kuwa, siku ya tukio hilo, juzi majira ya saa 4:15 asubuhi, Jaibu Nyoni (26) ambaye ni mhudumu wa Bar hiyo, alitoa taarifa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi kuwa askari Donald amelala kwenye kochi na amejaribu kumwamsha lakini imeshindikana.

Kamanda Marwa alifafanua zaidi kuwa, baadaye askari waliongozana na daktari kwenda eneo la tukio ambako walimkuta askari huyo akiwa amelala kwenye kochi ambalo liko ndani ya bar hiyo.

Marwa amesema katika uchunguzi ilibainika kuwa askari huyo alifika kwenye baa hiyo Machi 12, majira ya ... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More