ASKARI POLISI WATANO NA MWANAJESHI MMOJA WAFIKISHWA KORTINI WAKIKABILIWA NA KESI YA UHUJUMU UCHUMI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ASKARI POLISI WATANO NA MWANAJESHI MMOJA WAFIKISHWA KORTINI WAKIKABILIWA NA KESI YA UHUJUMU UCHUMI

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv.,
ASKARI Polisi watano na Mwanajeshi mmoja wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi yenye mashtaka matatu likiwamo la wizi wa mafuta ya ndege na Utakatishaji wa zaidi ya Sh. Milioni nne.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni Koplo Shwahiba(38), MT. 74164 SGT Ally Chibwana (47), wa jeshi la wananchi Tanzania, PC Elidaima Paranjo (38), PC Simon (28), PC Dickson na PC Hamza.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa na wakili wa serikali , Faraji Nguka akisaidiana na Saada Mohammed mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Mwaikambo imedai washtakiwa wote hao wakiwa ni watumishi wa umma walikiuka maadili ya kazi zao na kupanga genge la uhalifu na kuiba lita 2180 za mafuta ya ndege( Jet A-1/Ik yenye thamani ya sh. 4,647,760.
Katika shtaka la pili imedaiwa, Julai 30,2019 huko katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere uliopo katika Wilaya ya Ilala jijini Darvea Salaam, watuhumiwa hao(askari), waliiba lita 2180 za mafuta ya ndege( Jet A-1/Ik ... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More