Aslay Athibitisha, Kufanya Kazi kwa Kujitegemea Kuna Faida Kubwa. - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Aslay Athibitisha, Kufanya Kazi kwa Kujitegemea Kuna Faida Kubwa.

Msanii wa muziki wa bongo fleva , Aslay anasema kuwa kufanya azi kwa kujitegemea kuna utofauti mkubwa sana kuliko kufanya kazi kama kundi au kufanya kazi pamoja  kama ilivyokuwa kwake hapo awali.


Hata hivyo Aslay anasema kuwa pamoja na kwamba sasa hivi anafanya kazi peke yake lakini bado yupo karibu na wasanii wenzake waliokuwa wakiunda kundi lao la ya moto band lililovunjika mwaka uliopita.


Aslay anasema kuwa hakuna utofauti wala ugomvi kati yao na kama itatokea moja wao akitaka kufanya nae kazi atafanya nae lakini ameona kuna utofauti mkubwa sana kufanya kazi kama kundi na kufanya peke yake lakini pia anaamini kuwa kufanya kazi katika kundi ilikuwa ni moja ya safari yake ya kimuziki.


Itambulike kuwa hapo awali aslay na wenzake walikuwa wakifanya kazi pamoja kama kundi lakini baadae wwalikuja wakashindwana na kuanza kufanya kazi kila mmoja kwa kujitegemea.


 


The post Aslay Athibitisha, Kufanya Kazi kwa Kujitegemea Kuna Faida Kubwa. appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More