ATAKA KUJIUA KWA KUTUMIA WEMBE BAADA YA KUHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI MINNE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ATAKA KUJIUA KWA KUTUMIA WEMBE BAADA YA KUHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI MINNE

Dixon Busagaga, Rombo.
MTU mmoja aliyefahamika kwa majina ya Colman Massawe mkazi wa Rombo amenusurika kufa alipofanya jaribio la kujiua kwa kukata shingo yake kwa kutumia Wembe muda mfupi baada ya kuhukumiwa kwenda jela miezi minne.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Hamis Issah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Massawe alihukumiwa kwenda jela miezi minne baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya kuvunja nyumba usiku na kuiba .
“Jana (Juzi)  ilikuwa ni siku ya hukumu yake na alihukumiwa kwenda jela miezi minne, lakini cha ajabu  ni kwamba kijana huyo ambaye alitokea gerezani wakati wa kufikishwa mahakamani hapo, aliingiza mkono mfukoni na kutoa kiwembe kipya na kuanza kujichinja” alisema Kamanda Issah.
Kamanda Issah alisema tukio hilo lilitokea muda mfupi wakati askari wakimpeleka kwenye gari, tayari kupelekwa gerezani ndipo alipochukua uamuzi huo wa kujikata sehemu koromeo.... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More