ATAPE KUWEKEZA KWENYE MIRADI YA MAJI, UJENZI WA HOSTELI SIMIYU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ATAPE KUWEKEZA KWENYE MIRADI YA MAJI, UJENZI WA HOSTELI SIMIYU

Na Stella Kalinga, SimiyuChama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato(ATAPE), kinakusudia kuwekeza katika ujenzi wa mradi wa maji kuunga mkono juhudi za Serikali katika utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi na ujenzi wa hosteli ili kutoa huduma za malazi katika Mkoa wa Simiyu.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Freddie Manento, Aprili 17, 2019 wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi, ambako unafanyika Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama hicho kwa takribani siku saba ambao umeanza Aprili 16 na utahitimishwa Aprili 21, 2019.
Manento amesema ATAPE imedhamiria kuwekeza kwenye miradi itakayokuwa na tija kwa Watanzania wote kwa ujumla huku akieleza kuwa timu ya wataalam wa uwekezaji wa chama hicho inaendelea kufanya utafiti, ili kubaini eneo litakalofaa kuchimba kisima cha maji na kujenga hosteli mkoani Simiyu. “Tumedhamiria kuacha alama katika Mkoa wa Simiyu kupitia mku... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More