ATUMIA MSAFARA WA MAGARI YA WAOMBOLEZAJI KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ATUMIA MSAFARA WA MAGARI YA WAOMBOLEZAJI KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA

Na Rashid Nchimbi wa Polisi ArushaJeshi la Polisi mkoani hapa limemkamata kijana mmoja jina linahifadhiwa mkazi wa Daraja Mbili halmashauri ya jiji la Arusha akiwa na kilogramu 207 za dawa ya kulevya aina ya Mirungi.
Akitoa taarifa hiyo mapema leo ofisini kwake, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi alisema kwamba, mtuhumiwa huyo alikamatwa jana saa 6:00 Mchana akiwa anatokea mpakani mwa mkoa wa Kilimanjaro kuingia mkoa wa Arusha aliamua kutumia mbinu mpya ya usafirishaji wa dawa hazo kwa kujipachika katikati ya msafara wa magari yaliyokuwa yanakwenda msibani.
Kamanda Ng’anzi alisema kwamba Jeshi hilo lilipata taarifa juu ya uwepo wa mtu huyo aliyekuwa anasafirisha Mirungi kwa kutumia gari ndipo walipowapeleka askari haraka katika eneo la Kikatiti wilayani Arumeru na kuweka mtego.
“Wakiwa katika eneo hilo baada ya muda askari hao waliona gari aina ya Suzuki Escudo rangi ya Kijivu lenye namba za usajili T 505 CNC likiwa katik... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More