Aubameyang ang’ara, Arsenal yaishushia kipigo kitakatifu Vorskla Poltava - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Aubameyang ang’ara, Arsenal yaishushia kipigo kitakatifu Vorskla Poltava

Nyota wa klabu ya Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang hapo jana usiku ameng’ara kwenye michuano ya Europa League baada ya kufunga mabao mawili peke yake na kuisaidia timu yake kuchomoza na ushindi mujarabu wa 4-2 dhidi ya Vorskla Poltava.Akiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani, Auba mwenye umri wa miaka 29, alianza kuipatia bao la kwanza Arsenal dakika ya 32, kisha akafunga la pili dakika 56, huku Danny Welbeck akifunga dakika ya 48 na Mesut Ozil akiitimisha karamu ya magoli kwa bao lake safi dakika ya 74.


Wakati mabao mawili ya kufutia machozi ya Vorskla yakifungwa na nahodha wao Vladimir Chesnakov dakika ya 76 na Vyacheslav Sharpar (90+4) kabla mpira kumalizika.


Kikosi cha Arsenal, Leno (6), Sokratis (7), Lichtsteiner (6), Holding (7), Monreal (7), Elneny (6), Mkhitaryan (7), Torreira (7), Iwobi (7), Welbeck (7), Aubameyang (8).

Wachezaji wa akiba, Ozil (6), Guendouzi (6), Smith-Rowe (6).


Kikosi cha Vorskla Poltava, Shust (6), Perduta (5), Chesnakov (6), Dallku (5), De Souza (5), ... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More