Aunty Lulu Amshauri Diamond Afunge Ndoa - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Aunty Lulu Amshauri Diamond Afunge Ndoa

Muigizaji wa Bongo movie na Mtangazaji Lulu Semagongo maarufu kama Aunt Lulu ameibuka na kumtaka staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kuoa.


Aunt Lulu amedai kwamba kutokana na Diamond ameshakuwa mtu Mzima anaamini kuwa akioa kutamletea heshima sana katika jamii.


Kwenye mahojiano yake na gazeti la Risasi Jumamosi, Aunt Lulu alidai ameamua kumshauri staa huyo ambaye amekuwa akimpenda siku zote kutokana na kujituma kwake kikazi kwani si kila mwanamke ana nyota nzuri ya kumfanya aende mbali.Unajua ujana huwa hausubiri, kadiri unavyosherehekea siku yako ya kuzaliwa ndivyo uzee unavyokaribi, sasa kwa Diamond ili azeeke vizuri, angeoa sasa kwani Waswahili wanakwambia kubadilibadili wanawake nako huleta mikosi na kujikuta ukianguka moja kwa moja“.Aunt Lulu pia ameongeza kuwa akishaoa hata wanawake wanaojigonga kwake watapungua sana kwani ataheshimiwa.


The post Aunty Lulu Amshauri Diamond Afunge Ndoa appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More