AUSSEMS ASEMA HAMJUI NIYONZIMA, SIMBA SC KUMKOSA ASANTE KWASI MECHI NA NDANDA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AUSSEMS ASEMA HAMJUI NIYONZIMA, SIMBA SC KUMKOSA ASANTE KWASI MECHI NA NDANDA

Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
KOCHA Mbelgiji wa Simba SC, Patrick J Aussems amesema kwamba hamjui mchezaji wa klabu hiyo Mnyarwanda Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima.
Mbelgiji huyo ameyasema hayo leo jioni Uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam wakati wa mazoezi ya mwisho wa Simba SC kabla ya safari ya Mtwara kesho asubuhi kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Ndanda FC Jumamosi Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
“Ndiyo nani Haruna? Silijui hilo jina na sijawahi kulisikia tangu nimekuja hapa,”alisema Mbelgiji huyo aliyeanza kazi Julai akimpokea Mfaransa, Pierre Lechantre baada ya kuulizwa na Waandishi wa Habari juu ya kiungo huyo kutoonekana mazoezini leo timu ikijiandaa kwa safari ya Mtwara.

Haruna Niyonzima alijiunga na Simba SC msimu uliopita kutoka kwa mahasimu, Yanga SC

Mbali na Niyonzima, wachezaji wengine waliokosekana mazoezini Simba SC leo ni beki Juuko Murshid, kiungo Jonas Mkude waliopewa ruhusa kushughulikia masuala yao binafsi, Asante Kwasi ambaye ni m... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More