AUSSEMS AWAENGUA KIKOSINI COULIBALY, KWASI MECHI NA SAOURA JUMAMOSI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AUSSEMS AWAENGUA KIKOSINI COULIBALY, KWASI MECHI NA SAOURA JUMAMOSI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KOCHA Mbelgiji wa Simba SC, Patrick J. Aussems amewaondoa kwenye programu ya mchezo dhidi ya JS Saoura mabeki Zana Coulibaly kutoka Burkina Faso na Mghana Asante Kwasi.
Simba SC watakuwa wenyeji wa JS Saoura ya Algeria Jumamosi kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika.
Na kuelekea mchezo huo, Aussems amewaweka pembeni wachezaji wanane – pamoja na Coulibaly na Kwasi, wengine ni kipa Ally Salim, mabeki Paul Bukaba, Yusuph Mlipili, kiungo Mohamed ‘Mo’ Ibrahim na washambuliaji Abdul Suleiman na Adam Salamba.

Patrick Aussems amewaondoa Zana Coulibaly na Asante Kwasi kwenye mchezo dhidi ya JS Saoura

Wanane hao wanabaki Zanzibar na wataungana na kikosi cha timu ya vijana, Simba B kuendelea na michuano ya Kombe la Mapinduzi kuanzia hatua ya Nusu Fainali.
Wachezaji 18 wa Simba SC wamerejea leo Dar es Salaam kutoka Zanzibar baada ya timu kushinda mechi zote tatu za Kundi A Kombe la Map... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More