AWESO AAGIZA WATALAAM WA MAJI NA WAKANDARASI WA MIRADI YA MAJI YA TSAMAS NA DARAKUTA-MINJINGU WAITWE POPOTE WALIPO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AWESO AAGIZA WATALAAM WA MAJI NA WAKANDARASI WA MIRADI YA MAJI YA TSAMAS NA DARAKUTA-MINJINGU WAITWE POPOTE WALIPO

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ameelekeza Watalaam wa maji walioshiriki katika kusimamia ujenzi wa miradi ya maji ya Tsamas na mradi wa maji Darakuta-Minjingu pamoja na Wakandarasi waliopewa kandarasi katika miradi hiyo kufika katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Babati bila kukosa asubuhi ya tarehe 23.10.2018.
Mhe. Aweso (Mb) ambaye yuko mkoani Manyara katika ziara ya kikazi ametoa maelekezo hayo baada ya kubaini kasoro katika utekelezaji wa miradi hiyo ambapo pamoja na Serikali kutoa fedha, bado wananchi hawajapata huduma ya majisafi na salama.
Mradi wa maji wa Darakuta-Minjingu ambao hadi sasa umetumia kiasi cha Shilingi Bilioni 1.7 ulisanifiwa mwaka 2009 na ulitakiwa kuhudumia vijiji vya Minjingu, Mwada, Ngoley, Olasiti, Masaini, Maramboi na Eluwai. Aidha, mradi wa maji wa Tsamas mkandarasi amelipwa zaidi ya Shilingi milioni 100, hata hivyo mabomba yaliyotumika katika chanzo cha maji yanapasuka hivyo kusababisha ukosefu wa huduma ya majisafi ya uhakika kwa wananchi.
Naibu Waziri A... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More