AWESO AMLILIA RAIS MAGUFULI BARABARA YA TANGA,PANGANI SAADANI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AWESO AMLILIA RAIS MAGUFULI BARABARA YA TANGA,PANGANI SAADANI

SERIKALI ya awamu ya tano imeombwa kuangalia namna ya kuanza ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani, Saadan hadi Bagamoyo ili kuweza kumaliza kilio cha wananchi wa wilaya ya Pangani cha muda mrefu ikiwemo kufungua fursa za kiuchumi na maendeleo kwa mkoa . 
Ombi hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso wakati akizungumza kwenye mkutano wake wa hadhara wilayani humo ambapo alisema pamoja na kuwepo kwa miradi mingi inayotekelezwa huko lakini kilio kikubwa cha wananchi wake ni ukosefu wa barabara nzuri. 
Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) alisema wakati Rais Magufuli akiomba kura kwa wananchi hao mwaka 2015 aliwaahidi wananchi ujenzi wa barabara hiyo na walikubali kumpa kura nyingi na imani kubwa kwake kwa mategemeo ya kumpata mkombozi atakae weza kumaliza kero hiyo ambayo imedumu katika awamu zote nne zilizopita bila ya mafanikio. 
“Kwenye mkutano wangu wa leo hii nipo hapa nyumbani kama Mbunge wenu kawaida na sikuja kama Naibu Waziri na jukumu l... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More