AZAM FC WAJIGAMBA KUIFUNGA BIASHARA UNITED KATIKA MCHEZO WAO WA LEO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AZAM FC WAJIGAMBA KUIFUNGA BIASHARA UNITED KATIKA MCHEZO WAO WA LEO

Na Agness Francis, Globu ya jamii
UONGOZI wa Kikosi cha Azam chini ya  Kocha Mkuu wake Hans Van der Pluijm umesema kwa mazoezi waliyofanya sasa vijana  wapo tayari kupambana dhidi ya Biashara United.

Mchezo huo unatarajiwa kufanyika  leo saa 10 jioni katika dimba la Karume mkoani Mara.

Hivyo Azam mchezo huo wa leo ni wa nne  kwao katika Ligi Kuu Tanzania Bara na wanashika nafasi ya pili wakiwa na alama saba.

Wakati timu ya  Biashara ni  mzunguko wa tano na wanashika nafasi ya 12 ikiwa na alama nne.

Ambapo JKT Tanzania  wakiwa vinara wa ligi hiyo ambayo imeshacheza michezo 4 mpaka sasa na wakiwa na alama 8.

Katika mchezo uliopita Azam FC ilionesha kulazimisha sare  ya kufungana 1-1 dhidi  Mwadui FC katika uwanja wa Kambarage huko mkoani Shinyanga.

Wakizungumzia mchezo wa leo dhidi ya Biashara ,Uongozi wa Kikosi cha Azam umesema wachezaji wao wako vizuri na  hakuna majeruhi.

Wameongeza wachezaji wao kila mmoja akiwa na morali ya kuondoka na alama tatu  ugenini.... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More