AZAM FC YAAMUA KUZIRUDISHA UWANJA WA TAIFA MECHI ZAKE DHIDI YA VIGOGO, SIMBA NA YANGA SC - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AZAM FC YAAMUA KUZIRUDISHA UWANJA WA TAIFA MECHI ZAKE DHIDI YA VIGOGO, SIMBA NA YANGA SC

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imehamishia rasmi Uwanja wa Taifa mechi zake za nyumbani itakazocheza na Simba na Yanga kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu huu.
Katika barua iliyoandikwa jana na kusainiwa na Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat' kuelekea Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB) na nakala yake kutumwa kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imeeleza kuwa sababu kubwa ya Azam FC kufikia uamuzi huo ni kuwapa nafasi mashabiki wengi kushuhudia mechi hizo kutokana na udogo wa Uwanja wa Azam Complex.
“Uongozi wa Azam Football Club unaomba ofisi yako tukufu kurejesha mechi zetu za Ligi Kuu za nyumbani zinazohusisha timu za Simba na Yanga zichezwe katika Uwanja wa Taifa msimu huu 2018/2019 badala ya kuchezwa Uwanja wa wetu wa Azam Complex,” amesema Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin​ 'Popta' katika barua hiyo.
Ikieleza sababu za kufikia uamuzi huo, barua hiyo iliyoandikwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abd... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More