AZAM FC YAIFUATA MWADUI FC SHINYANGA MECHI YA KWANZA YA UGENINI LIGI KUU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AZAM FC YAIFUATA MWADUI FC SHINYANGA MECHI YA KWANZA YA UGENINI LIGI KUU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC Alfajiri ya leo imeondoka kwenda Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa ajili ya mchezo dhidi ya wenyeji, Mwadui FC.
Azam FC itakipiga na Mwadui kwenye Uwanja wa Mwadui Ijumaa hii saa 8.00 mchana, ambapo baada ya mchezo huo itakuwa na kibarua kingine Musoma kuvaana na Biashara United Septemba 19 kabla ya kuelekea jijini Mwanza kumenyana na Alliance Septemba 23.
Msafara wa Azam FC umeondoka na wachezaji wote walio fiti kikosini, wakiwemo nyota saba waliokuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa, nahodha Aggrey Morris na msaidizi wake, Frank Domayo, David Mwantika, Mudathir Yahya, Yahya Zayed waliokuwa Taifa Stars.

Wengine wawili ni kiungo mshambuliaji Tafadzwa Kutinyu (Zimbabwe) na Nickolas Wadada (Uganda).
Kuelekea mechi hizo tatu, Kocha Mkuu wa Azam FC, Hans van der Pluijm, amesema kuwa amekipanga kikosi chake kwa ajili ya ushindi huku akidai atakuwa na siku mbili za kukiweka sawa kikosi ... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More