AZAM FC YAKUTANA NA KIPIGO KIKALI UGANDA, YAFUNGWA 4-2 NA KCCA LUGOGO - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AZAM FC YAKUTANA NA KIPIGO KIKALI UGANDA, YAFUNGWA 4-2 NA KCCA LUGOGO

Na Mwandishi Wetu, KAMPALA
AZAM FC imepoteza mchezo wa kwanza leo katika ziara yake ya Uganda baada ua kuchapwa mabao 4-2 na wenyeji, KCCA Uwanja wa klabu hiyo uliopo eneo la Lugogo mjini Kampala, Uganda.
Azam FC inayofundishwa na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm anayesaidiwa na mzalendo, Juma Mwambusi ilitangulia kwa mabao ya beki Aggrey Morris dakika ya tatu na mshambuliaji mpya, Daniel Lyanga dakika ya sita.
Lakini KCCA wakazinduka na kusawazisha mabao hayo ndani ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Muzamil Mutyaba dakika ya 15 na Timoth Awanyi dakika ya 44, kabla ya kuongeza mengine mawili kipindi cha pili kupitia kwa Allan Kyambadde dakika ya 48 na Patrick Kaddu dakika ya 69.

Huo ulikuwa ni mchezo wa pili katika kambi yake ya Uganda kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, baada ya awali kulazimishwa sare ya 0-0 na URA Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala. ... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More