AZAM FC YAPANIA KUIPIGA TANZANIA PRISONS KESHO UWANJA WA SOKOINE - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AZAM FC YAPANIA KUIPIGA TANZANIA PRISONS KESHO UWANJA WA SOKOINE

Na Mwandishi Wetu, MBEYA
KIKOSI cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, tayari kimewasili salama mkoani Mbeya kikiwa kimejidhatiti kufanya kweli kwenye mchezo ujao dhidi ya Tanzania Prisons.
Azam FC inawasili mkoani humo ikiwa imetoka kucheza mkoani Iringa dhidi ya Lipuli jana Jumatatu, ikipata sare ya bao 1-1 huku bao lake likifungwa na kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
Akizungumza leo mjini hapa, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Juma Mwambusi, aliwapongeza wachezaji kwa kutoka nyuma na hatimaye kupata sare ya ugenini.
Juma Mwambusi, aliwapongeza wachezaji kwa kutoka nyuma na hatimaye kupata sare ya ugenini na Lipuli
Kocha Mkuu, Mholanzi Hans van der Pluijm akiongoza mazoezi leo

Mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma akiwa mazoezini leo

“Mchezo ulikuwa ni mzuri na mgumu, Azam kipindi cha kwanza hatukuweza kucheza vizuri kwa sababu wachezaji waliingia kwenye mchezo wakiwa na kasi ya chini, kwa kiasi kikubwa ilichangiwa na hali ya uwanja kwa sababu ilinyesha mvua kabla ya mpira ku... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More