AZAM FC YASAJILI MCHEZAJI MPYA KUTOKA IVORY COAST ALIKUWA ANACHEZA GHANA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AZAM FC YASAJILI MCHEZAJI MPYA KUTOKA IVORY COAST ALIKUWA ANACHEZA GHANA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, umekamilisha taratibu za kumsajili kiungo mshambuliaji, Richard Djodi, kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa usajili huru akitokea kwa vigogo wa Ghana, Ashanti Gold.
Huo ni usajili wa mwisho kwa Azam FC kwa ajili ya msimu ujao, ikiwa hadi sasa imesajili wachezaji wapya watano, watatu wakiwa wa kigeni na wawili wazawa.
Djodi raia wa Ivory Coast, anayemudu kucheza nafasi zote za ushambuliaji, alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 17 na pasi 13 za mwisho, katika mechi 35 alizoichezea Ashanti Gold huku katika mechi 12 za mwisho akipiga manne.
Wachezaji wengine wapya waliosajiliwa na Azam FC chini ya Kocha Mkuu mpya, Mrundi Etienne Ndayiragijje ni Idd Suleiman 'Nado', Suleimani Ndikumana, Emmanuel Mvuyekure na Abalkasim Khamis.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat' akibadilishana mikataba na Richard Djodi

 Kwa sasa kikosi cha Azam FC kipo mjini Kigali, Rwanda kinaposhiriki michuano ya Klabu Bingwa Afri... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More