AZAM FC YASHINDWA KUTWAA TENA KOMBE LA KAGAME, YAPIGWA 1-0 NA KCCA KIGALI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AZAM FC YASHINDWA KUTWAA TENA KOMBE LA KAGAME, YAPIGWA 1-0 NA KCCA KIGALI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya KCCA ya Uganda imefanikiwa kutwaa taji la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC ya Dar es Salaam Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali leo.
Bao lililoipa ushindi huo Timu ya Mamlaka ya Jiji la Kampala limefungwa na Mustafa Kiiza dakika ya 62 aliyemtungua kipa Mghana wa Azam FC, Razack Abalora kwa shuti la mguu wa kushoto. 
Kwa ushindi huo, KCCA wamezawadiwa dola za Kimarekani 30,000, huku washindi wa pili, Azam FC wakipewa kifuta jasho cha dola 20,000 na washindi wa tatu, Green Eagles ya Zambia dola 10,000.

Nahodha wa Azam FC, Mzimbabwe Bruce Kangwa akikabidhiwa mfano wa hundi ya dola 20,000 baada ya kufungwa na KCCA leo katika fainali

Ushindi huo unamaanisha KCCA wanatwaa taji lao la pili tu la kombe la Kagame kihistoria baada ya awali kulitwaa mwaka 1978 ilipoifunga Simba ya Tanzania pia katika fainali.
Aidha, kwa ushindi huo KCCA wameendeleza ubabe wao kwa Azam FC baada ya kuilaza 1-0 pia Julai... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More