Azam fc yatamba kumgaragaza mnyama simba fainali kagame cup - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Azam fc yatamba kumgaragaza mnyama simba fainali kagame cup

Na Agness Francis, Globu ya jamii
Azam fc yatamba kumgaragaza mnyama simba katika fainali za kuwania kombe  la kagame cup (cecafa).
Timu hizo zote mbili za kutoka hapa nchini ambazo zimefanikiwa kutinga fainali zitashuka dimbani kesho majira ya saa 12 jioni kuchoshana nguvu  katika uwanja wa taifa Jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya jana azamfc kumuondosha gor mahia ya nchini kenya  katika michuano hiyo  kwa kipigo cha  mabao 2-0, sasa wanakutana na wekundu wa msimbazi katika kumjua nani ataibuka kidedea wa kombe hilo.
Akizungumza leo jijini Dar es  salaam msemaji wa Azam FC Jaffary Iddi Maganga amesema  kuwa kikosi chao kimejipanga vizuri kuhakikisha wanatetea ubingwa  wao wa mwaka 2015 ambapo  michuano hiyo ilifanyika kwa mara ya mwisho hapa nchini. 
Jaffary amesema maandalizi waliyofanya ni mazuri na ndio maana wamefanya vema  na mpka kufikia hatua hiyo.
"Tunaiheshimu simba ni timu kongwe ya muda mrefu ilio na kikosi mahiri lakini sisi azam tunaliamini benchi letu la ufundi pamo... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More