AZAM FC YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA KAGAME, KAZI IMEBAKI KWA KMC KESHO - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AZAM FC YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA KAGAME, KAZI IMEBAKI KWA KMC KESHO

Na Mwandishi Wetu, KIGALI
TIMU ya Azam FC imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame pamoja na kulazimishwa sare ya 0-0 na Bandari ya Kenya katika mchezo wa mwisho wa Kundi B leo Uwanja wa Huye mjini Butare.
Sare hiyo inaifanya Azam FC inayofundishwa na kocha Mrundi, Etienne Ndayiragijje imaliza na pointi nne kufuatia kushinda 1-0 dhidi ya Mukura Victory na kufungwa 1-0 na KCCA katika mechi zake mbili za awali.
Mechi nyingine ya kundi hilo leo, KCCA iliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Mukura Victory hapo hapo Uwanja wa Huye. 
Mabao ya KCCA yalifungwa Mike Mutyaba dakika ya tano na Allan Okello dakika ya 42, wakati la Mukura Victory lilifungwa na Gael Duhayindavyi.

Mshambuliaji wa Azam FC, Obrey Chirwa (kushoto) akimpita mchezaji wa Bandari leo mjini Kigali

Azam FC imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Kagame 

Sasa KCCA inamaliza na pointi saba kileleni mwa kundi ikifuatiwa na Azam FC yenye poi... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More