AZAM FC YATOKA NYUMA NA KUITANDIKA STAND UNITED 3-1 CHAMAZI NA KUENDELEA KUIKARIBIA YANGA KILELENI LIGI KUU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AZAM FC YATOKA NYUMA NA KUITANDIKA STAND UNITED 3-1 CHAMAZI NA KUENDELEA KUIKARIBIA YANGA KILELENI LIGI KUU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya Azam FC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Stand United mabao 3-1 usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
Baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza timu hizo zikimaliza bila kufungana, kipindi cha pili Stand United walitangulia kwa bao la Hafidh Mussa dakika ya 53, kabla ya Azam FC kutokea nyuma na kuibuka na ushindi huo.
Alianza kiungo Mghana, Enock Atta-Agyei kuisawazishia Azam FC dakika ya 66 kabla ya mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Yahya Zayed kufunga mfululizo dakika ya 72 kwa penalti na 85.

Yahya Zayed akishangilia baada ya kufunga mabao mawili leo dhidi ya Stand United

Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 36 baada ya kucheza 14, ikiendelea kukamata nafasi ya pili nyuma ya Yanga SC, yenye pointi 38 za mechi 14 pia.
Mabingwa watetezi, Simba SC wanafuatia katika nafasi ya tatu kwa pointi zao 27 za mechi 12 wakiwa na viporo viwili kutokana na kukabiliwa ... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More