AZAM KUONYESHA CHANELI ZA NDANI BURE - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

AZAM KUONYESHA CHANELI ZA NDANI BURE

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amelieleza Bunge leo Jumanne Mei 14, 2019 kuwa kituo cha televisheni cha Azam jana Jumatatu kimepokea leseni ya kuonyesha chaneli za ndani bure.

Naibu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye  alipotembelea TCRA
Pia, Nditiye amesema katika kipindi cha miezi saba watajenga mfumo wa kurusha chaneli hizo, hivyo wananchi wanapaswa kuvuta subira.

Naibu waziri ametoa kauli hiyo akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, aliyehoji ni kwa nini Azam wananyimwa haki ya kuonyesha channel za ndani bure.

"Je, Serikali haioni kuwanyima haki hiyo wakati wengine wamepewa ni kukiuka ibara ya 18 ya katiba ambayo inatoa haki ya kupata habari, lakini hata Rais wetu anatumia Azam kurusha matangazo yake hivyo tungejitangaza hadi nje," ameuliza Shangazi.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Nyamagana (CCM), Stanslaus Mabula, aliuliza Serikali iwapo haioni kupitia TCRA kuwafungia local channels (chanel z... Continue reading ->
Source: Mwanaharakati MzalendoRead More