Azam yapokea kichapo kibaya mbele ya KCCA nchini Uganda - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Azam yapokea kichapo kibaya mbele ya KCCA nchini Uganda

Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC imekubali kipigo cha mabao 4-2 dhidi ya KCCA katika mchezo wa kirafiki wa maandalizi ya msimu ujao.Mchezo huo uliofanyika Uwanja wa KCCA, benchi la ufundi Azam FC la iliutumia kama sehemu ya kujiweka sawa baada ya mazoezi makali ya takribani siku 10 kambini nchini Uganda.


Azam FC ilianza vema mchezo huo kwa kujipatia mabao mawili ya haraka, ikianza kufunga la kwanza dakika ya tatu lililofungwa na nahodha Agrey Moris, kwa mkwaju wa penalti.


Penalti hiyo ilitokana na mshambuliaji wa Azam FC, Danny Lyanga, kuangushwa ndani ya eneo la 18 na nahodha wa KCCA, Timothy Awany.


Dakika ya sita, Lyanga alitupia bao la pili kwa shuti la chini akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na beki wa kushoto, Bruce Kangwa.


Kuelekea dakika 29 za mwisho za kipindi cha kwanza, KCCA ilifanikiwa kusawazisha mabao yote kupitia kwa Muzamiru Mutyaba dakika ya 16 na Awany dakika ya 45 na kufanya mchezo kwenda mapumziko kwa sare ya 2-2.


Azam FC ilirejea kipindi cha pili ... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More