Baada ya Alikiba kuzindua MoFaya, Nandy naye ajitosa kwenye ujasiriamali aja na bidhaa hizi (+video) - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Baada ya Alikiba kuzindua MoFaya, Nandy naye ajitosa kwenye ujasiriamali aja na bidhaa hizi (+video)

Ikiwa ni wiki mbili zimepita tangu msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba kuzindua kinywaji  chake cha Mofaya, hatimaye msanii mwingine wa muziki, Mrembo Nandy naye amejitupa kwenye ujasiriamali.


Nandy amesema kuwa ameingia ubia na kampuni ya Grace Products inayojihusisha na utengenezaji wa sabuni za kuogea na vipodozi mbali mbali vya asili na yeye atakuwa ni moja ya wamiliki wa kampuni hiyo.


Akifunguka kuhusu dili hilo leo Mei 17, 2018 mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam, Nandy amesema bidhaa zote za vipodozi na sabuni vitakuwa na jina na picha zake na kuwataka mashabiki wake wamuunge mkono kwa kununua bidhaa zake.

Loading...Jiunge na Bongo5.com sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More