BAADA YA KUREJEA CCM MGEJA AENDA MBUGA ZA WANYAMA KUONDOA 'STRESS' - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BAADA YA KUREJEA CCM MGEJA AENDA MBUGA ZA WANYAMA KUONDOA 'STRESS'

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii 

SIKU chache baada ya kurejea Chama Cha Mapinduzi(CCM) Hamisi Mgeja amesema ameamua kwenda kuondoa 'Stress' katika mbuga za wanyama za Ngorongoro na Serengeti.

 Mgeja aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga amerejea Chama hicho mwanzoni mwa wiki iliyopita akitokea Chadema ambapo alijiunga na chama hicho wakati wa mchakato wa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

 Akizungumza leo kwa njia ya simu Mgeja ameiambia Michuzi Blog kuwa kwa sasa wameamua kwenda kujipumzisha mbuga za wayama baada ya kurejea CCM na hiyo inatoa nafasi kwake na wenzake kutafakari maisha mapya ndani ya CCM baada ya kurejea tena.

"Baada ya kumaliza kazi ya kumsindikiza Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa  nyumbani Monduli na kupokelewa na maelfu ya Wananchi wa Mkoa wa Arusha na Wana-CCM katika tukio la kurejea kwake rasmi na kupewa kadi mpya.

"Tumeamua kuja mbuga za wanyama kupumzika kidogo, ni wakati sahihi kwetu kuondoa 'Stress' za Chadema wakati tunafakari namna ya kushiri... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More