Baada ya kusajiliwa Chirwa afunguka ‘Azam wasipo nipa changu navunja mkataba, timu ya Msuva inanitaka’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Baada ya kusajiliwa Chirwa afunguka ‘Azam wasipo nipa changu navunja mkataba, timu ya Msuva inanitaka’

Klabu ya Azam FC imekubali kumsajili Mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia na mchezaji wa zamani wa Yanga, Obrey Cholla Chirwa kwa mkataba wa mwaka mmoja.Wakati akitambulishwa mbele ya waandishi wa habari, Chirwa amesema kuwa wachezaji wengi wa Tanzania hawana msimamo huku akimwagia sifa Samatta kuwa amefanikiwa kutokana na msimamo wake hivyo hatoweza kuvumilia endapo atakosa haki zake ndani ya klabu.


”Wachezaji wa Tanzania hawana msimamo, mfano Samatta yeye anamsimamo hivyo na mimi ninamsimamo wangu kama mtu hanipi kitu changu ninachostahili navunja mkataba hapo hapo,” amesema Chirwa.


Obrey Cholla Chirwa ameongeza ”Hata Azam wasipo nipa naweza kuvunja mkataba nitasubiri nini naweza kuvunja kwasababu nina familia na inanitegemea hata wewe mwandishi familia inakutegemea unafanya kazi,” amesema hayo alipoulizwa na mwandishi wa habari.


”Kwa hiyo kama klabu inashindwa kunilipa kutokana na makubaliano yetu, naomba mikataba yangu niondoke kuna timu inanitaka Misri nimekataa timu Si... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More