Baada ya Marekani na UK, Rayvanny kukisanua Tanzania - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Baada ya Marekani na UK, Rayvanny kukisanua Tanzania

Msanii wa muziki Bongo kutoka WCB, Rayvanny amefunguka sababu ya kufanya show nyingi zaidi nje kuliko Bongo.


Muimbaji huyo amesema kinachopelekea hilo ni kutokana waandaji wengi wanaojitokeza ni kutoka nje ya nchi ila kuna mpango wa kufanya tour Tanzania.


“Namshukuru Mungu nilikuwa na tour UK, Marekani lakini pia nina mpango mwaka huu kuwa na tour nyingine, kuna watu ambao tumeongea nao kuna mipango ya kufanya Tanzania nzima,” Rayvanny ameiambia Bongo5.


“Show nyingi tunafanya sana nje sijajua ni sababu gani lakini inatokea hivyo lakini mwaka huu nitafanya tour Tanzania baada ya kumaliza Marekani,” ameongeza.


Rayvanny kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Pochi Nene’ ambayo amemshirikisha producer S2kizzy.

Loading...Jiunge na Bongo5.com sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More