BAADHI YA WANANCHI WADAI VIGUTA MAMILIONI YA FEDHA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BAADHI YA WANANCHI WADAI VIGUTA MAMILIONI YA FEDHA

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 
WANANCHI zaidi ya 200 mkoani Pwani,wanadai kutapeliwa fedha milioni 185 ,kwa ajili ya kupatiwa viwanja na kujengewa nyumba kwa gharama nafuu kupitia kampuni ya Vicoba group union Tanzania (VIGUTA). 
Aidha Chamwino huko Dodoma wanadai kuidai kampuni hiyo milioni 61 huku wakikosa kupatiwa nyumba walizolipia kujengewa kwa gharama nafuu.
Aliyekuwa meneja wa Viguta mkoani Pwani,Iddi Kanyalu alikiri kuwepo kwa tetesi hizo na kudai taarifa hizo tayari amezifikisha kwenye vyombo vya sheria ili kufanya uchunguzi na sheria kufuata mkondo wake. 
Alisema,ni kweli walikuwa wananchi wanalipia viwanja kwa bei nafuu na nyumba walikuwa wakilipia kwa asilimia 25 mfano ukitaka kujengewa nyumba ya milioni 25 unalipia milioni 7.5 ambapo wengi walishalipia asilimia 25 na wengine fedha zote kisha kuingizwa mkenge. 
Kanyalu alieleza, utapeli huo umegusa watu ambao wameuziwa viwanja hewa na nyumba ambazo hawajakabidhiwa hadi sasa. 
"Wamenisababishia doa, kwanza mimi ni diwani wa kata ya... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More