BABA MATATANI KWA KUMBAKA NA KUMLAWITI BINTI YAKE - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BABA MATATANI KWA KUMBAKA NA KUMLAWITI BINTI YAKE


Mahakama ya Wilaya ya Temeke imemsomea maelezo ya awali mshtakiwa Haruna Abdu (54) mkazi wa Mbagala Mwanamtoti kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti binti yake wa kumzaa (12).
Akisoma maelezo hayo mwendesha mashataka, Salome Assey alisema kuanzia Januari mwaka 2017 hadi Februari 2019 mshtakiwa alikuwa akimbaka mwanaye wa kumzaa na kumuingilia kinyume na maumbile.
Amesema ilipofika Februari 2019, mtoto huyo alishindwa kwenda shule kutokana na vitendo alivyofanyiwa na mzazi wake huyo.
Alisema alipohojiwa na mwalimu wake aliyefahamika kwa jina la Ngulula, mtoto huyo alimueleza kuwa alikuwa anafanyiwa vitendo hivyo na baba yake ndipo taarifa ilipotolewa kituo cha polisi.
Ameongeza kuwa baada ya hapo, mtoto huyo alipewa fomu namba 3 ya Polisi (PF3) kwa ajili ya uchunguzi wa hospitali na baada ya hapo uliandaliwa mtego kwa ajili ya kumkamata mshtakiwa.
Aliongeza kuwa Machi 4, 2019 wakati mshtakiwa anarudi nyumbani akitokea kazini alikamatwa na polisi akiwa anataka kumbaka bintiye.
“Aliporudi nyumba... Continue reading ->Source: Mwanaharakati MzalendoRead More