BABU MPYA KAMA WA LOLIONDO AIBUKA DAR, APIGA KAMBI SOKO LA FERI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BABU MPYA KAMA WA LOLIONDO AIBUKA DAR, APIGA KAMBI SOKO LA FERI

*Unanunua chupa ya maji anachanganya na dawa zake*Wengine watoa ushuhuda, awekea ulinzi ili asisumbuliwe
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii BABU mwingine kama Babu wa Loliondo aibuka Dar! Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Mganga wa kienyeji aliyetambulika kwa jina moja la Yakub kuanza kutoa huduma ya kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu kwa kutumia dawa anayoweka kwenye chupa ya maji ya kunywa.
Mganga huo ameanza kujizolea umaarufu na hasa unapofika sokoni hapo ambapo mbali ya kuwa na idadi kubwa ya watu wanaosubiri kupata dawa yake , pia wapo ambao wameitumia na kupona wamekuwa wakitoa ushuhuda kuwa wamepona.
Mwandishi wa Michuzi Blog amepata nafasi ya kushuhudia na kuona namna ambavyo watu wamejazana wakisubiri kupata huduma kutoka kwa mganga huyo.Gharama ya dawa zake ni Sh.3000.
Hata hivyo changamoto kubwa ni namna ya kumfikia hasa kwa mtu ambaye anafika eneo hilo kwa ajili ya kutaka kuzungumza naye .
Wingi wa watu umesababisha mganga huyo kulindwa na askari wa SUMA JKT katika kuhakikisha anakuwa salama wakati wote pindi anapotoa huduma zake.
Kwa mujibu wa watu ambao wamepata nafasi ya kutumia dawa za mganga huyo wamemsifu kwa madai dawa zake zinasaidia kwani wamepona.
Akizungumza leo na Michuzi Blog jijini Dar es Salaam, Said Katuma ambaye ni moja ya watu ambao wanamsaidia mganga huyo katika kutoa huduma zake anasema wameweka utaratibu mzuri utakaohakikisha wote wanaofika hapo wanapata dawa.
Mganga aliyejulikana kwa jina laYakub akitoa huduma kwa wananchi waliojitokeza kwenye soko la samaki la feri jijini Dar es Salaam leo Septemba 13,2018.Chupa za maji ya kunywa zikiwa zimechanganywa na dawa ya Mganga Yakub kabla ya kukabidhi kwa wahusika jijini Dar es Salaam leo.Kusoma zaidi BOFYA HAPA.


Source: Issa MichuziRead More