Babu Tale Adai Hata Akichepuka Mke Wake Hawezi Kumuacha - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Babu Tale Adai Hata Akichepuka Mke Wake Hawezi Kumuacha

Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale maarufu kama Babu Tale amefunguka na kudai kuwa anajua hata akichepuka mke wake hawezi kumuacha.


Wikiendi iliyopita Babu Tale alisafiri kwenda nchini South Africa kwa ajili ya kuwapatanisha Diamond na mzazi Wenzake Zari baada ya kutokiwa Kwenye maelewano kwa miezi kadhaa.


Lakini tangu akiwa S.A kumekuwa na  taarifa Mtandaoni zinazodai kuwa Babu Tale amezaa mtoto na mwanamke mwingine na kumtelekeza mtoto huyo bila matunzo yoyote.


Baada ya taarifa hizo watu walimjia juu Babu Tale kwa kukimbilia kurekebisha maisha ya Diamond ilihali ya ndoa yake na mkewe  yanamshinda.


Basi Babu Tale kawamwagia povu wale wote wanaoeneza taarifa na kusema yeye na mke wake wametoka mbali wako pamoja kwa zaidi ya miaka 17 hivyo mke wake hawezi kumuacha hata afanye kosa gani.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram Babu Tale alimwaga povu hili: 


The post Babu Tale Adai Hata Akichepuka Mke Wake Hawezi Kumuacha appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More