BABU WA LOLIONDO AUNGANISHWA NA UMEME WA REA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BABU WA LOLIONDO AUNGANISHWA NA UMEME WA REANa Ahmed Mahmoud Ngorongoro
MCHUNGAJI mstaafu wa kanisa la KKKT, ambae kwa sasa anatoa huduma ya matibabu ,Ambilikile Mwaisapile, ameipongeza serikali kwa kuwasha umeme nyumbani kwake na kusema kuwa sasa amepata mwanga atafanya kazi zake hata nyakati za usiku tofauti na hali ilivyokuwa kabla ya kupata umeme.
Mchungaji Mwaisapile maarufu babu Kikombe wa Samunge, wilayani Ngorongoro,ameyasema hayo jana nyumbani kwake mara baada ya waziri wa Nishati Dakta Medadi Kalemani, kuwasha umeme wa REA nyumbani kwake.
Mwaisapile, amesema hakutegemea kama kuna siku angelipata Umeme lakini sasa ameishukuru serikali kwa kumuwashia umeme wa Rea, nyumbani kwake.
Amesema kutokana na serikali kutekeleza miradi ya umeme Vijiji Tanzania itakuwa ni kioo cha maendeleo barani Afrika.
Akizindua na kuwasha umeme huo Waziri wa Nishati,Dakta Kalemani, amesema serikali ipo katika kutekleza miradi ya umeme vijijini kupitia REA,na kurejea maelekezo yake kwa wakandarasi kuhakikisha hakuna Kitongoji ,Kijiji,Kata ambayo ny... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More