BAJETI 2019/2020: KODI YA 'MAWIGI' KUPANDA, MUDA WA LESENI KUONGEZWA, KUFUTWA MSAMAHA WA KODI KWENYE TAULO ZA KIKE, NK - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BAJETI 2019/2020: KODI YA 'MAWIGI' KUPANDA, MUDA WA LESENI KUONGEZWA, KUFUTWA MSAMAHA WA KODI KWENYE TAULO ZA KIKE, NK


Hayo yamesemwa Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akiwa anatoa mapendekezo ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020
Amesema "Napendekeza kuongeza muda wa leseni za udereva kutoka miaka mitatu ya sasa hadi miaka mitano, napendekeza kuongeza tozo ya leseni ya udereva kutoka Tsh. 40,000 kwenda Tsh. 70,000."
Hata hivyo ameongeza kuwa Napendekeza kuongeza ada ya usajili wa magari 10,000 hadi 50000, bajaji kutoka 10,000 hadi 30,000 na pikipiki kutoka 10,000 hadi 20,000
Aidha katika hatua nyingine amesema kuwa "Napendekeza kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye nywele za bandia zinazotengenezwa nchini na asilimia 25 kwenye nywele bandia zinazoagizwa kutoka nje ya nchi, lengo la hatua hii ni kuongeza mapato ya Serikali."
Pia aliongelea Kufutwa kwa msamaha kodi ya ongezeko la thamani kwenye taulo za kike kwa kuwa haujawezesha kupatikana kwa bei nafuu kwa bidhaa hiyo muhimu kwa walengwa, badala yake ni kuwanufainisha wafanyabiashara. 
Hadi April 2019 Serikali imetoa Tril 5.4 k... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More