BAKHRESA ATOA NDEGE YAKE BINAFSI KWA MARA YA KWANZA IWABEBE WACHEZAJI WA AZAM FC - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BAKHRESA ATOA NDEGE YAKE BINAFSI KWA MARA YA KWANZA IWABEBE WACHEZAJI WA AZAM FC

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MFANYABIASHARA Bilionea, Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa kwa mara ya kwanza jana alitoa ndege yake binafsi na familia yake iwabebe wachezaji klabu yake, Azam FC mjini Bukoba.
Walikuwa ni wachezaji wake walioitwa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ili wawahi kurejea Dar es Salaam kujiunga na wenzao kwa safari ya Afrika Kusini kambini.
Hiyo ilikuwa mapema jana, yaani baada tu ya mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar walioshinda 1-0, bao pekee la mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma.
Ndege ya Bilionea, Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa ikiwa Uwanja wa Ndege wa Bukoba jana na wachezaji wa Azam FC

Wachezaji hao ni mabeki Aggrey Morris, Abdallah Kheri, viungo Mudathir Yahya, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na mshambuliaji Yahya Zayed.
Lakini pia katika ndege hiyo walikuwepo wachezaji wengine wa timu za taifa za nje, beki wa Uganda Nico Wadada na kiungo wa Zimbabwe, Tafadzwa Kutinyu waliokuja kuunganisha ndege Dar es Salaam kwenda kujiun... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More