BALAA LINGINE LAFANYIKA MSIMBAZI, MO AVUNJA BENKI - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BALAA LINGINE LAFANYIKA MSIMBAZI, MO AVUNJA BENKI


WANANUKA fedha! Ndiyo utakavyoweza kusema kwa wachezaji wa Simba baada ya kupewa shilingi milioni 300 na mwekezaji wao bilionea, Mohammed Dewji ‘Mo’ kufuatia kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hiyo, ikiwa ni siku moja tangu timu hiyo ifuzu katika hiyo michuano mikubwa Afrika kwa kuwafunga wapinzani wao AS Vita mabao 2-1 mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, mabao ya Simba yalifungwa na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Mzambia, Clatous Chama huku lile la Vita likipachikwa na Kasadi Kasengu.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo limezipata Championi Jumatatu, wachezaji hao watapewa mamilioni hayo baada ya ushindi wa michezo mitatu ya hatua ya Robo Fainali katika Kundi D lenye timu nne.

Mtoa taarifa huyo alisema wachezaji hao waliahidiwa kupewa Sh milioni 100 kwa kila mchezo watakaoshinda na kutokana na kushinda michezo mitatu, basi watachukua Sh milioni 300.

Aliongeza kuwa, wachezaji hao awali waliahidi w a kupewa Sh milioni 100 ... Continue reading ->

Source: Mwanaharakati MzalendoRead More