Balozi aipokea Simba DR Congo - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Balozi aipokea Simba DR Congo

Msafara wa wachezaji 19 wa klabu ya Simba umewasili Kinshasa Congo DR kwa ajili ya mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya AS Vita.


Safari ilianza asubuhi (saa 2:50) kutoka Dar na kuwasili saa 7 mchana (kwa saa za Congo DR) sawa na saa 9 kwa Afrika Mashariki.Msafara umepokelewa na balozi wa Tanzania nchini Congo DR Luteni Jenerali mstaafu, Paul Ignac  Mella.


“Napenda kutumia fursa hii kuwapongeza kwa vile mmejiandaa vizuri nimeona mechi yenu ya kwanza mlipocheza na timu ya Algeria (JS Saoura) mlicheza vizuri sana na kuiweka nchi yetu kwenye ramani nzuri sana”-Luteni Jenerali mstaafu, Paul Ignac  Mella.“Kutokana na uchezaji wenu mahiri, tutaendelea kuwa na nyie na kuwaunga mkono, msiwe na wasiwasi hali ya hapa ni salama kama mlivyoona hakuna vita na hatutegenei vita.”


“Congo nao wanajua Kiswahili kama sisi kwa hiyi wapo pia watawashangilia kwa hiyo msishangae mkiona washangiliaji wamekuwa wengi.”Nahodha wa Simba John Bocco hakuambatana na timu kwa... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More