Balozi Dr. Abdallah Possi, awasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Hungary Bw. János Áder - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Balozi Dr. Abdallah Possi, awasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Hungary Bw. János Áder

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dr. Abdallah Possi, aliwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Hungary Bw. János Áder hivi karibuni. Pamoja na Ujerumani, Ubalozi wa Tanzania uliopo Berlin pia unahudumia maeneo mengine tisa tisa ya uwakilishi, ikiwemo nchi ya Hungary.  Baada ya kuwasilisha hati, Balozi alipata fursa ya mazungumzo mafupi na Rais wa Hungary, mazungumzo ambayo yalilenga zaidi katika masuala ya kilimo, elimu na maji. Balozi Dkt. Possi alimueleza Rais wa Hungary kwamba Tanzania inawakaribisha wawekezaji katika maeneo mbalimbali, yakijumuisha pia viwanda vinavyojihusisha na mazao ya kilimo. Dkt. Possi alifafanua kwamba, kilimo ni sekta ambayo bado inategemewa na watanzania walio wengi, na kwamba kuna fursa nyingi zaidi katika sekta ya kilimo siyo tu kutokana na uwepo wa ardhi nzuri yenye rutuba, bali pia uwepo wa idadi kubwa ya watu ndani ya Tanzania na nchhi zinazoizunguka, hali ambayo inahakikisha uwepo wa soko la uhakika katika bidhaa za kilimo. Dkt. Possi al... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More