Balozi Mgaza aahidi kuandaa mafunzo zaidi kwa wataalam wa afya nchini - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Balozi Mgaza aahidi kuandaa mafunzo zaidi kwa wataalam wa afya nchini

 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto, Abdulhakiem Kattan wa Saudia Arabia akizungumza kabla ya shughuli ya utoaji vyeti kwa washiriki wa mafunzo ya kusimamia upumuaji kwa wagonjwa wa ICU. Daktari Bingwa wa Watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Evelyne  Assenga akikabidhiwa cheti na Balozi wa Tanzania nchini Saudia Arabia, Hemedi Iddi Mgaza baada ya kumalizika kwa mafunzo ya kusimamia upumuaji kwa wagonjwa wanaolazwa ICU. Wengine katika picha ni wataalam wa afya kutoka Saudia Arabia. 
Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo leo, balozi huyo amesema wataendelea kuandaa mafunzo ya huduma za afya kwa wataalam mbalimbali nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo. 
Kauli hiyo imetolewa leo na balozi huyo wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili kuhusu upumuaji kwa wataalam kutoka hospitali mbalimbali nchini ikiwamo Bugando, Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Hospitali ya Benjamini Mkapa na Hospitali ya Mkoa wa Dodoma. 
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More