Balozi Seif afuturu na wazee wanaoishi nyumba za serikali Zanzibar - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Balozi Seif afuturu na wazee wanaoishi nyumba za serikali Zanzibar

Waumini wa Dini ya Kiislamu Nchini wanaendelea na harakati zao za kufutari pamoja zinakopelekea kushibana kiimani ya moyo ndani ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, mwezi ambao umeteremshwa Kitabu Kitakatifu cha Quran kisichoshaka katika kubainisha Haki na Batil.
Futari hizo zinazojumuisha Waumini wa rika tofauti ufanywaji wake hupaswa kuzingatia utaratibu maalum wa hali ya Kiafya na Mazingira safi uliowekwa na Uongozi wa Manispaa pamoja na Halmashauri za Wilaya.
Futari hiyo iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi iliwahusisha Wazee wanaohifadhiwa kwenye Nyumba za Serikai Sebleni pamoja na Wazee wa Chama cha Mapinduzi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja na kufanyika katika Ukumbi wa Nyumba za Wazee Sebleni Mjini Zanzibar.
Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed alisema Balozi Seif bado anaendeleza tabia njema ya kuwashirikish... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More