Balozi Seif akutana na Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama kutoka Nchini India - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Balozi Seif akutana na Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama kutoka Nchini India

Na Othman Khamis/Rashida Abdi, OMPRMakamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amekutana kwa mazungumzo ya Timu ya Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama kutoka Chuo cha Kijeshi Nchini India.
Timu hiyo iliyoongozwa na Balozi Mdogo wa India aliyepo Zanzibar Bwana T.B Barual ipo Tanzania kujifunza mambo mbali mbali ikiwemo masuala ya Historia ya Uhuru wa Tanganyika na Ukombozi wa Zanzibar.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ukumbi wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar Balozi Seif  aliushauri Uongozi wa Timu hiyo kuandaa utaratibu maalum wa kuwapatia Mafunzo ya muda mfupi ama mrefu Maafisa na Wapiganaji wa Vikosi Maalum vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema India na Tanzania ikiwemo Zanzibar kwa ujumla Zina historia  ndefu katika masuala ya Kisiasa, Uchumi, Utamaduni na Biashara ambayo kwa sasa upo umuhimu wa kuelekeza nguvu hizo katika masuala ya Ulinzi ili Amani iendelee kutawala ndani ya Ukanda wa Bahari ya Hindi.
Nao kwa upande wao Maka... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More