Balozi Seif aongoza matembezii ya miaka 55mya Mapinduzi ya Zanzibar - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Balozi Seif aongoza matembezii ya miaka 55mya Mapinduzi ya Zanzibar

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema Vijana walioshiriki matembezi ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar wanapaswa kujenga ufahamu wa kujuwa Mapinduzi ndio yaliyoleta Ukombozi na kupatiana Mamlaka kamili ya Mwafrika yanayoharakisha Maendeleo ya Jamii hivi sasa.
Alisema jukumu la Vijana hao kwa wakati huu waelewe kwamba Uhuru wa Taifa hili wakati wowote utalindwa na wao wenyewe kwa vile hakuna Mtu au Kikundi kitakachokuja Zanzibar na Tanzania Nzima  kuwalindia Uhuru walioachiliwa kama urithi wao.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akiyapokea na kuyafunga Matembezi ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi {UVCCM} ya kuunga mkono Mapindui ya Zanzibar ya Mwaka 1964 yaliyohitimishwa hapo katika Uwanja wa Gombani ya Kale Chake Chake Kisiwani Pemba.
Alisema Vijana hao ndio warithi halali wa Mapinduzi hayo kwa sababu Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 yalifanywa na Vijana chini ya Viongozi wa ASP Youth Leagae kwa wakati huo wakitekeleza... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More