Balozi Seif aweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la shule ya Sekondari ya Uweleni kisiwani Pemba - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Balozi Seif aweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la shule ya Sekondari ya Uweleni kisiwani Pemba

Wazanzibar wana kila sababu ya kujivunia Maendeleo makubwa yaliyopatikana katika Sekta ya Elimu yaliyosimamiwa na Chama cha Afro Shirazy Party  na Baadae CCM katika kipindi chote cha  Miaka 55 tokea kufanyika kwa Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 yaliyoondoa Utawala wa Kibaguzi katika Elimu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Skuli ya Sekondari ya Uweleni iliyopo Mkoani Kisiwani Pemba katika Smra shamra za kusherehekea Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar  ya Mwaka 1964 kutimia Miaka 55.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hatua iliyofikia Taifa hivi sasa katika Sekta ya Kielimu ni kubwa kiasi kwamba wale wanaokebehi wanashindwa kujifahamu kwamba wanajidharau wao wenyewe  na dawa yao ni kupuuzwa kwa sababu hawajui thamani ya kuwa na chao na wala sio watu wanaothamini cha wenzao. Alisema tokea Wananchi wa Zanzibar walipojitawala  kutoka katika makucha ya kibeberu, Vijana wa Visiwa hivi wanaende... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More