BALOZI SEIF AZINDUA KITUO CHA TAIFA CHA KUWAHUDUMIA WALEMAVU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BALOZI SEIF AZINDUA KITUO CHA TAIFA CHA KUWAHUDUMIA WALEMAVU

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati umefika kwa Serikali Kuu kwa kushirikiana na Taasisi na Mashirika megine ya Kitaifa na Kimataifa kujenga Kituo cha Taifa kitakacholenga kuwahudumia Watu wenye ulemavu katika kuwajengea nguvu na maarifa ya kuendelea kujitegemea Kimaisha.
Alisema Ulimwengu wa sasa umebadilika kwa kubeba harakati nyingi zinazoibua matukio mbalimbali yanayosababisa Jamii kukumbwa na ajali tofauti  katokana na kasi ya maisha na hatimae kuzalisha Walemavu wanaohitaji huduma za matunzo na maarifa mengine ya Kimaisha.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa hafla maalum ya kuzindua rasmi Kituo cha Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu cha Jimbo la Shaurimoyo kiliopo pembezoni mwa Skuli ya Sekondari ya Ufundi Mikunguni Mjini Zanzibar.
Alisema tabia ya kuwatenga Watu wenye Ulemavu haipendezi na nidhambi jambo ambalo halikubaliki katika Jamii yoyote ile. Hivyo aliwahimiza wahusika hao wasikubali kukata tamaa katika kupigania haki zao.
Makamu wa Pili ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More