BALOZI SEIF: UJIO WA MASHUA YA MAZINGIRA NI DARASA KWA WANANCHI WALIOWENGI NCHINI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BALOZI SEIF: UJIO WA MASHUA YA MAZINGIRA NI DARASA KWA WANANCHI WALIOWENGI NCHINI


Rais wa Taasisi inayosimamia mazingira ya Umoja wa Mataifa Bwana Siim Valmar Kiislar amesema wakati umefika kwa Mataifa yote Ulimwenguni kuwa na mfumo Mmoja unaoeleweka wa utunzaji wa Mazingira utakaosaidia kuifanya Dunia iendelee kubakia salama.

Bwana Siim Valmar Kiislar alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Ofisi yake iliyomo ndani ya Jengo la Baraza la Wawakilishi liliopo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Zanzibar bado inaendelea kuathirika na mabadiliko ya Tabia Nchi akatolea mfano ufukwe wa Bahari ya Msuka uliopo kaskazini mwa Kisiwa cha Pemba ambao tayari umeshaliwa na mawimbi ya Bahari kwa sehemu kubwa.

Balozi Seif aliueleza Ujumbe huo ujio wa mashua ya Mazingira katika Visiwa vya Unguja na Pemba utasaidia mfano wa Darasa kwa Wananchi waliowengi kuwa na muelekeo wa jitihada za mapambano dhidi ya mabadiliko ya Tab... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More