BALOZI SOKOINE AFUNGUA MAFUNZO YA WAWEZESHAJI WA MASHAMBA DARASA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BALOZI SOKOINE AFUNGUA MAFUNZO YA WAWEZESHAJI WA MASHAMBA DARASA

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Balozi Joseph Sokoine leo amefungua Mafunzo ya Msasa ya Uwezeshaji kuhusu Mashamba darasa kwa Maafisa viungo wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame nchini (ldfs), katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Morogoro.
“Ni matumaini yangu kuwa elimu na ufahamu mtakauopata kupitia mafunzo haya, mtaitumia katika kufanikisha uanzishaji wa mashamba darasa katika maeneo ya mradi” alisema Balozi Sokoine. Mafunzo hayo ya siku 5 yanalenga kujenga uwezo kwa washiriki katika uanzishaji wa mashamba darasa katika vijiji na shehia ambako mradi wa LDFS unatekelezwa.
Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wamekuwa wakitekeleza miradi inayolenga kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo kwa kusogeza karibu teknolojia kwa wakulima. Lengo likiwa ni kuongeza usalama wa chakula na kuongeza kipato cha jamii. Mradi wa L... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More