BALOZI WA KUWAIT AKABIDHI VIFAA TIBA KWA HOSPITALI KIGAMBONI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BALOZI WA KUWAIT AKABIDHI VIFAA TIBA KWA HOSPITALI KIGAMBONI

 Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, leo tarehe 10/6/2018 amepokea ugeni wa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najem.
Mapema akimkaribisha mgeni wake, DC Mgandilwa amemshukuru Balozi Najem kwa moyo wake wa upendo kwa  watanzania hususani wakazi wa Kigamboni. 
Ameeleza kuwa vifaa ambavyo vimetolewa ni vya zaidi ya Shilingi milioni kumi na moja na vinalenga kuondoa changamoto iliyokuwepo katika wodi za akina mama na watoto. 
Vifaa vilivyopokelewa ni pamoja na mashine za kusaidia wakati wa upasuaji, mashine za kusaidia kupumua, vifaa vya kupima moyo, vitanda vya watoto na beseni maalum kwa ajili ya akina mama wanaojifungua. 
DC Mgandilwa amesema kuwa nchi ya Kuwait ni miongoni mwa nchi ambazo ni marafiki wazuri wa Tanzania na kuwa Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kigamboni itaendeleza ushirikiano huo mwema. Kwa upande wake, Balozi Jasem Al Najem amewapongeza viongozi wa wilaya ya Kigamboni kwa ushirikiano mzuri ambao wamekuwa wakimpatia mara zote alipotembelea wilaya hiyo. 
B... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More