BALOZI WA MISITU NCHINI ATUMA SALAMU KWA VIJANA KUTAMBUA THAMANI YA MISITU...TFS NAO WAGUSIA MAPAFU YA DAR ES SALAAM YANAVYOHARIBIWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BALOZI WA MISITU NCHINI ATUMA SALAMU KWA VIJANA KUTAMBUA THAMANI YA MISITU...TFS NAO WAGUSIA MAPAFU YA DAR ES SALAAM YANAVYOHARIBIWA


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
BALOZI wa Misitu nchini ambaye pia ni Miss Tanzania namba mbili Nelly Kazikazi amewashauri Watanzania wote nchini na hasa vijana kushiriki kikamilifu katika kutunza misitu iliyopo nchini huku akisisitiza kuna kila sababu ya kuwa na utaratibu kwa kila mmoja wetu kupanda miti.
Wakati Balozi wa Misitu akihamasisha upandaji miti, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umesisitiza kuendelea na mkakati wake wa kuhakikisha inarejesha misitu ya asili katika maeneo ambayo imeharibiwa kwa kupanda miti ya asili kadri inavyowezekana ukiwemo Msitu wa Pugu ambao ndio mapafu ya Jiji la Dar es Salaam.
Hayo yameelezwa jana kwa nyakati tofauti baada ya kupandwa kwa miti zaidi ya 300 ya asili aina ya Mkakangazi katika Msitu wa Pugu mkoani Pwani. Wakati wa upandaji huo wa miti mbali ya kuwepo kwa maofisa wa TFS na Balozi wa Misitu, pia walikuwepo wadau wengine ambao ni wanafunzi wa Shule ya IST ya jijini Dar es Saalam.
Akizungumzia umuhimu wa kupanda miti, Balozi wa Misitu N... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More