Balozi wa Tanzania China Azitaka Taasisi za Umma Kuchangamkia Masoko China - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Balozi wa Tanzania China Azitaka Taasisi za Umma Kuchangamkia Masoko China

Na Beatrice Lyimo - MAELEZO, CHINA
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa  Kairuki amezitaka Taasisi zenye dhamana ya kutafuta masoko ya bidhaa mbalimbali nchini ikiwemo TANTRADE , Bodi ya Kahawa, Bodi za Chai, Korosho, Nafaka na Mazao mchanganyiko kushiriki kwenye maonesho mbalimbali yatakayofanyika nchini China ili kutafuta masoko mapya ya bidhaa zao. Balozi Kairuki ameyazungumza hayo alipokutana na ujumbe wa Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi walipotembelea nchini China kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu baina ya China na Tanzania katika tasnia ya habari na mawasiliano.
"Uzoefu wa hivi karibuni umekuwa wa kukatisha tamaa kutokana na Ubalozi kutafuta fursa mbalimbali kwa ajili ya bidhaa za Tanzania kutangazwa lakini wadau wameshindwa kushiriki" ameongeza Balozi Kairuki. Aidha, Balozi Kairuki amesema kuwa kumekuwepo na ongezeko la matumizi ya kahawa miongoni mwa Watu wa Jamhuri ya China na kahawa ya Tanzania ni miongoni mwa kahawa zinazopendwa sana na watu hao... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More