Bandari kiwira kuongeza Mapato hadi shilingi 3.6bn/- kwa mwaka - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Bandari kiwira kuongeza Mapato hadi shilingi 3.6bn/- kwa mwaka

Na Humphrey Shao, KyelaUpanuzi wa bandari ya Kiwira iliyopo wilayani Kyela mkoani Mbeya unatarajia kuongeza mapato ya bandari za Ziwa Nyasa kutoka wastani wa Sh milioni 300 kwa mwaka hadi kufikia Sh bilioni 3.6.
Hayo yameelezwa na Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa, Abeid Galus, wakati akizungunza na waandishi wa habari waliofika kuangalia Miradi ya Maendeleo inayofanywa na mamlaka ya bandari katika Ziwa Nyasa.
"Upanuzi huu unahusisha ujenzi wa sakafu ngumu katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 11,000 ambalo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi makaa ya mawe tani 10,000 kwa wakati mmoja.  Upanuzi huo utaongeza kasi ya upakuaji wa meli tofauti na sasa ambapo meli husubiria malori yanayobeba makaa ya mawe kupeleka viwandani" amesema Galusi.
Amesema kwa sasa meli moja yenye uwezo wa tani 1000 inatumia siku tisa kushusha mzigo badala ya siku moja kama ukishushwa eneo na kuhifadhia wakati ukisubiri malori ya kuubeba.
"Ujenzi huu wa eneo la kuhifadhia mizigo utaiongezea bandari mapato kwa zaidi ya mara... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More